37. Dalili ya thelathini na tano kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


37- Abul-´Izz Muhammad bin Muhammad bin Mawaahib al-Khuraasaaniy ametukhabarisha: Abul-Husayn bin at-Twuyuuriy ametuhadithia: Muhammad bin ´Aliy bin al-Fath al-Harbiy ametuhadithia: Abu Hafsw bin Shaahiyn ametuhadithia: Muhammad bin Makhlad ametuhadithia: ´Abdus bin Bashiyr ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdil-Waahid al-´Asqalaaniy ametuhadithia: Abu Nu´aym ´Umar bin Subh ametuhadithia, kutoka kwa Muqaatil bin Hayyaan, kutoka kwa adh-Dhwahhaak bin Muzaahim, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Allaah ana nguzo ya nuru inayoanzia kwenye mbingu ya saba mpaka juu kwenye ´Arshi. Wakati mja anaposema “Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah”basi nguzo ile inatikisika ambapo Allaah anasema: “Tulia.”Inasema: “Ee Mola! Ni vipi nitatulia na Wewe hujamsamehe aliyesema hivo?” Ndipo Allaah (Ta´ala) anasema: “Nimekwishamsamehe.” Hakikisheni mnaitikisa nguzo hiyo kwa wingi.”[1]

[1] Imezuliwa  kwa mujibu wa Ibn-ul-Jawziy katika ”al-Mawdhuu´aat” (3/166). adh-Dhahabiy amesema:

”Ibn Hibbaan amesema kwamba ´Umar bin Subh anazua Hadiyth.” (Tartîb-ul-Mawdhû´ât (277))

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 128-129
  • Imechapishwa: 18/06/2018