37. Dalili ya matarajio


Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya matarajio ni maneno Yake (Ta´ala):

فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

“Hivyo anayetaraji kukutana na Mola wake, basi atende tendo jema na wala asishirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote.”

MAELEZO

Matarajio ni mtu kuwa na matarajio kwa kitu kilicho karibu kupatikana. Vilevile inaweza kuwa inahusiana na kitu ambacho kupatikana kwake kuko mbali, lakini kwa fikira zake kikawa karibu.

Matarajio yanayoambatana na udhalilifu na unyenyekevu hayafanyiwi yeyote isipokuwa Allaah (´Azza wa Jall). Kumfanyiwa yeyote asiyekuwa Allaah (Ta´ala), huzingatiwa ima ni shirki ndogo au kubwa kutegemea na kilichomo ndani ya moyo wa yule mwenye kutaraji. Mtunzi wa kitabu ametumia dalili maneno Yake (Ta´ala):

فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

“Hivyo anayetaraji kukutana na Mola wake, basi atende tendo jema na wala asishirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote.”

Tambua kuwa matarajio yenye kusifiwa hayawi isipokuwa kwa yule mwenye kumtii Allaah na huku akitarajia thawabu za Allaah au ametubu kwa madhambi yake na huku akatarajia kukubaliwa tawbah yake. Ama matarajio pasi na matendo, ni chochote isipokuwa kudanganyika na matarajio batili na yenye kusemwa vibaya.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 57-58
  • Imechapishwa: 22/05/2020