37. Dalili ya kwamba nyoyo za waumini zimefunguliwa na nuru ya Allaah

37- Sa´iyd bin ´Abbaas ametuhadithia: ´Ubayd bin Muhammad ad-Daqqaaq ametuhadithia Baghdaad: al-Firyaabiy ametuhadithia: Sulaymaan bin ´Abdir-Rahmaan ad-Dimashqiy… ح Muhammad bin ´Uthmaan bin an-Najm ametuhadithia: al-Husayn bin Ahmad ametuhadithia: Muhammad bin al-Musayyab ametuhadithia: Abuu ´Iysaa ametuhadithia: Ayyuub bin Suwayd ametuhadithia… ح ´Abdul-Jabbaar ametuhadithia: Ibn Mahbuub ametuhadithia: Abuu ´Iysaa ametuhadithia: al-Hasan bin ´Arafah ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Abbaas ametuhadithia… ح ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Muhammad al-Mukattab na wengine wametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Ahmad al-Mulhidiy ametuhadithia: Ibn Maniy´ ametuhadithia: Daawuud bin Abiy Hind ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Abbaas ametuhadithia: Yahyaa bin Abiy ´Amr ash-Shaybaaniy ametuhadithia: Sulaymaan bin ´Abdir-Rahmaan amesema: “Abuu Zur´ah Yahyaa bin Abiy ´Amr ash-Shaybaaniy ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdullaah bin ad-Daylamiy, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) aliumba uumbaji Wake kwenye usiku. Akawatupia sehemu katika nuru Yake. Mwenye kupatwa na nuru hiyo huongoka na mwenye kuikosa hupotea. Kwa ajili hiyo nasema kuwa kalamu imekauka kwa yale aliyoyajua Allaah (´Azza wa Jall).”[1]

[1] Ahmad (2/176), at-Tirmidhiy (2642) aliyesema kuwa ni nzuri, Ibn Abiy ´Aaswim (242-243) na al-Haakim (1/30) ambaye kaisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Swahiyh na nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (242-243).

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 76
  • Imechapishwa: 13/02/2017