37. Allaah hana mwanzo wala mwisho

Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Hana mwanzo wala mwisho.

MAELEZO

Amesema (Jalla wa ´Alaa):

هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

“Yeye ndiye wa Mwanzo na wa Mwisho na Aliye juu na Aliye karibu – Naye juu ya kila jambo ni mjuzi.” [1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wewe ndiye wa Kwanza; hakuna kabla yako kitu. Wewe ndiye wa Mwisho; hakuna baada yako kitu. Wewe ndiye Mwenye kudhihiri; hakuna juu Yako kitu. Wewe ndiye Mwenye kujificha; hakuna chochote chenye kufichikana Kwako.”[2]

Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) yuko juu ya viumbe Wake, Mwenye kudhibiti juu ya waja Wake, na hakuna kitu chenye kufichikana Kwake:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَخْفَىٰ عَلَيْهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ

“Hakika Allaah hakifichiki Kwake chochote katika ardhi wala katika mbingu.”[3]

[1] 57:3

[2] Muslim (2713).

[3] 3:5

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 32
  • Imechapishwa: 26/07/2021