37. al-´Ayyaashiy upotoshaji wa kumi wa al-Baqarah

al-´Ayyaashiy amesema:

“al-Fadhwl bin Swaalih amepokea kutoka kwa baadhi ya marafiki zake kuhusiana na Kauli Yake:

قُولُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ

“Semeni: “Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Ishaaq na Ya’quwb na kizazi chao…” (02:136)

“Neno “Semeni” inahusu watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama kuhusiana na Kauli:

فَإِنْ آمَنُوا بِمِثْلِ مَا آمَنتُم بِهِ فَقَدِ اهْتَدَوا

“Basi wakiamini kama vile mlivyoyaamini nyinyi, basi kwa yakini watakuwa wameongoka.” (02:137)

inahusu watu wengine wote.”

Salaam ameeleza kuwa Abu Ja´faar amesema kuhusu Kauli Yake:

آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا

“Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu…”

“Hamaanishi mwingine isipokuwa ni ´Aliy, al-Hasan, al-Husayn na Faatwimah na inawahusu maimamu baada yao.”[1]

Kwa mujibu wa mapokezi wa kwanza yuko wapi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam) na Maswahabah zake waumini? Kwa mujibu wa mapokezi ya pili yuko wapi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah zake watukufu na watu wa familia ya Mtume tokea wakati ule mpaka hii leo? Ni upotoshaji namna gani! Ni uchezaji wa ki-Baatwiniy namna gani kwa maandiko ya wazi ya Qur-aan! Allaah (Ta´ala) Amesema kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake:

فَإِنْ آمَنُوا بِمِثْلِ مَا آمَنتُم بِهِ

“Basi wakiamini kama vile mlivyoyaamini nyinyi… “

Bi maana makafiri katika mayahudi, manaswara na wengine. Inawalekea wale waumini wenye kuamini Vitabu na Mitume wote pasina kufarikanisha mmoja katika wao:

فَقَدِ اهْتَدَوا

“… basi kwa yakini watakuwa wameongoka…”

Bi maana watakuwa wameongozwa katika haki:

وَّإِن تَوَلَّوْا

“… na wakikengeuka…”

Bi maana wakigeuzia haki mgongo na kuchagua batili baada ya kufikiwa na haki:

فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ ۖفَسَيَكْفِيكَهُمُ اللَّـهُ

“… hakika wao wamo katika upinzani, basi Allaah Atakutosheleza nao.”

Bi maana Atakunusuru juu yao – Naye ni Mwenye kusikia, mjuzi.”

Kwa msemo mwingine Aayah imeanza ikimwelekea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na waumini wote. Halafu Aayah ikaisha kwa kumwelekea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo ameahidiwa nusura na ushindi juu ya wale wenye kumkufuru Allaah na Mtume Wake.

[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/61-62).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 70-71
  • Imechapishwa: 19/03/2017