36. Wudhuu´ kwa mwanamke anayetokwa na utoko nyakati zote

Swali 36: Anapotawadha mwanamke anayetokwa na utoko wenye kuendelea kwa ajili ya swalah ya faradhi – je, inafaa kwake kuswali swalah ya Sunnah na kusoma Qur-aan kwa wudhuu´ wa faradhi hiyo mpaka kutapoingia faradhi ya pili?

Jibu: Akitawadha kwa ajili ya kuswali swalah ya faradhi mwanzoni mwa wakati basi inafaa kwake kuswali atakayo katika swalah za faradhi na za Sunnah na kusoma Qur-aan mpaka pale kutapoingia wakati wa swalah nyingine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 34
  • Imechapishwa: 01/08/2021