36. Waabudu makaburi wametumbukia katika matendo ya mayahudi na manaswara

Watu hawa wametumbukia katika yaleyale waliyotumbukia mayahudi na manaswara kwa kujengea juu ya makaburi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika waliokuwa kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya Mitume wao na watu wao wema kuwa ni mahali pa kuswalia. Tanabahini! Msiyafanye makaburi kuwa ni mahali pa kuswalia. Hakika mimi nakukatazeni na hilo.”[1]

Hili lilikuwa ni jambo linalokatazwa katika kizazi cha kwanza katika zama zaa karne bora. Hili lilikuwa linakatazwa na hapakukuwa kitu katika kuyajengea makaburi mpaka ilipokuja dola ya Faatwimiyyuun ya Shiy´ah na wakatawala huko Misri na nchi nyingi. Walikuwa Shiy´ah Baatwiniyyah. Wakajenga makuba juu ya makaburi. Watu wa kwanza kuyajenga ilikuwa ni Shiy´ah Baatwiniyyah. Kisha makaburi yakaenea katika miji ya waislamu baada ya hapo kwa sababu ya kitendo cha Shiy´ah. Allaah awakebehi. Wao ndio wa mwanzo kuyajengea makaburi, kama alivosema Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah).

[1] Ameipokea Muslim (532).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 61-62
  • Imechapishwa: 06/08/2018