36. Ni nani ambaye ana haki ya kuwaua Khawaarij?

Swali 36: Wasia wa kuwaua Khawaarij pale aliposema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mtapokutana nao basi waueni.”

kunapata kufahamu kupitia dalili hii na nyenginezo zilizofahamisha hivyo kwamba inajuzu kwa mtu yeyote yule katika Ahl-us-Sunnah kuwaua au wanaozungumzishwa ni kundi maalum katika waislamu?

Jibu: Ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba Khawaarij ni wazushi na wapotevu. Lakini hata hivyo haijuzu kwa yeyote kuwaua. Kazi hiyo ni ya watawala ambao wana utawala mikononi mwao. Lau tutasema yeyote anayekutana nao basi awaue, jambo hilo litapelekea katika vurugu. Maneno haya hayasemi mwanachuoni yeyote. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mtapokutana nao basi waueni.”

Wanaozungumzishwa hapa ni watawala, wale wenye utawala mikononi mwao na wale wenye kuzuia madhara kwa watu. Hawa ndio wanaozungumzishwa.

Kwanza inatakikana kwa nchi ambayo iko na Khawaarij kuwatumia mtu wa kujadiliana nao na awabainishie haki.

Pili wakikataa na wakaendelea na wasikubali baada ya hapo, wafanywe kile kinachowezekana kufanyiwa.

Ama kusema mtu amuue mwengine tu moja kwa moja, hili ni kosa. Ni wajibu kwanza kuwalingania. ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) hakuwapiga vita isipokuwa baada ya kuwalingania kwanza na akawatumia binamu yake ´Abdullaah bin ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na akamwambia:

“Jadiliana nao kwa Sunnah. Wana mtazamo fulani juu ya Qur-aan.”

Akajadiliana nao na wakarejea idadi ya watu wengi na wakabaki wenye kunaki. Kisha baada ya hapo pindi walipomuua ´Abdullaah bin Khabbaab na mjakazi wake (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ndipo ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) akawaendea na kuwaambia:

“Wametufanyia uasi kwa kumuua ´Abdullaah bin Khabbaab na mjakazi wake. Wote wakaitikia kuwa wamemuua.”

Pindi alipowalingania baada ya hapo na wakakataa ndio akawaua. Kuua ndio inakuwa jambo la mwisho pindi kunapokuwa hakuna tena matumaini ya kuwanyoosha kwa njia ambayo mtu anaweza kutumia kupitia mtawala. Baada ya hapo mambo yakipelekea kuwapiga vita wanapigwa vita.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 23/07/2017