36. Ni ipi hukumu ya swawm za pamoja?


Swali 36: Ni ipi hukumu ya swawm za pamoja, swalah za  pamoja na ´ibaadah kama hizo?

Jibu: Hii ni katika madhambi mazito. Sisi tunawajua watu hawa ambao wanawawajibishia watu mambo ambayo Allaah hakuwawajibishia. Wanafanya hivo kwa njia ya kutaka kupendezesha na wanaita kuwa ni “swalah za pamoja” na mengineyo. Sisi tunawajua watu hawa na tunazijua hali zao zilivyo. Watu wote wanawafahamu. Kitendo hichi ni batili. Mwenye kuamrisha hilo amejifanya mwenyewe kuwa ni muweka Shari´ah pamoja na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na amewajibisha kitu ambacho hakikuwajibishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwenyewe hakumuamrisha mtu kusimama usiku wala kufunga baadhi ya siku.

Watu hawa ni juu yao kumcha Allaah na kutubia kwa yale wanayoita “swawm za pamoja”, “swalah za pamoja” na mfano wa hayo. Haijuzu kabisa. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةُ الْفَصْلِ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۗ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Je, wanao washirika waliowaamuru dini yale ambayo Allaah hakuyaidhinisha? Kama si neno la uamuzi, ingelikidhiwa baina yao  – na hakika madhalimu watapata adhabu yenye kuumiza.” (42:21)

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 52-53
  • Imechapishwa: 12/06/2017