Miongoni mwa haki za mke juu ya mume wake asimsuse isipokuwa kukiwepo sababu inayopelekea kumsusa kwa lengo la kumtia adabu. Pindi itapokuwa imeruhusiwa kwa mwanaume kumsusa mke wake, basi amsuse nyumbani kwake [ndani] na si nyumba yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema wakati alipotaja haki za mwanamke kwa mume wake:

“… na wala asimsuse isipokuwa nyumbani.”[1]

[1] Abu Daawuud (2142), Ibn Maajah (1850), Ibn Hibbaan (9/2764), al-Haakim (2/2764) na Ahmad (4/446-447). Mnyororo ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Haakim na adh-Dhahabiy ameafikiana na hilo na hali kadhalika al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2033).

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 55
  • Imechapishwa: 24/03/2017