36. Hakitoki kitu nje ya matakwa na utashi wa Allaah

Maneno yake:

“Hakitoki kitu nje ya utashi Wake.”

Katika ulimwengu huu. Hakutokei kitu katika ukafiri, imani, utiifu, maasi, utajiri, uhai, kifo au riziki isipokuwa kwa matakwa Yake (Subhaanahu wa Ta´ala). Matakwa Yake ni yenye kuenea. Utashi Wake ni wenye kuenea. Kila kitu ni kwa utashi na matakwa Yake. Si kama wanavosema Mu´tazilah kwamba waja ndio wanaojiumbia matendo yao na kwamba Allaah kwayo hana athari yoyote kwa sababu wao wenyewe ndio wanaojiumbia matendo yao. Wanamsifia Allaah (Jalla wa ´Alaa) kushindwa na kumkanushia uumbaji na kutenda na kumjaalia waungu wengine pamoja Naye. Walio kinyume nao ni Jabriyyah wanaosema kuwa waja hawana uwezo wa kutenda na kwamba ni matendo ya Allaah ambaye anawapeleka kama kinavyopelekwa kifaa. Wanaona kuwa hawana matakwa wala utashi. Wao wako kinyume na Mu´tazilah.

Jabriyyah wamechupa mpaka katika kuthibitisha matendo ya Allaah na wamechupa mpaka katika kukanusha matendo ya waja na wamesema kuwa waja hawana uwezo wa kutenda. Kwa hiyo wamevuka mpaka katika kuthibitisha na katika kukanusha. Qadariyyah na Mu´tazila wako kinyume ambapo wamepindukia katika kuthibitisha matendo ya waja. Ni pande mbili zinazogongana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 56-57
  • Imechapishwa: 18/03/2021