36. Dunia hii ni jela ya muumini na pepo ya kafiri

222- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Dunia ni jela ya muumini na Pepo ya kafiri.”[1]

223- Dunia hii imekuwa ni kama jela kwa muumini kwa sababu amefungwa kwa majukumu. Hawezi akatikisika wala akatulia isipokuwa kwa hukumu za Shari´ah. Hapo ndipo anaweza ima kufanya au kuacha. Ukiongezea juu ya hilo anatiwa katika majaribio na mitihani mbalimbali. Katika muda huu ambao amefungwa anahisi khofu ya hali ya juu na wasiwasi. Kwa sababu hajui ahatihimisha katika hali gani.

Upande mwingine kafiri yuko huru kufungwa na majukumu. Hana wasiwasi wowote na mambo yaliyotajwa. Amezama katika matamanio yake na anakula raha na dunia na kudanganyika na masiku yake. Anakula na kupata raha kama mnyama. Tahamaki anaamka kutoka katika ndoto hizi na kujikuta katika jela ambayo hakufikiria.

224- Sahl as-Sa´luukiy all-Khuraasaaniy al-Hanafiy alikuwa ni katika viongozi wa dini na dunia. Siku moja alipokuwa akisindikizwa kwenda nyumba ya kuogelea myahudi mmoja akiwa na nguo za kuchanikachanika na zilizolowa akatoka nje ya nyumba na akasema: “Nyinyi si ndo mmepokea kutoka kwa Mtume wenu:

“Dunia ni jela ya muumini na Pepo ya kafiri.”?

Mimi ni mtumwa kafiri na unaiona hali yangu inavyofanana.” as-Sa´luukiy akamwambia: “Pindi kesho utapopata adhabu ya Allaah ndio utaona kuwa hii ilikuwa ni Pepo yako. Na pindi mimi nitapopata neema na radhi za Allaah ndio nitaona kuwa hii ilikuwa ni jela yangu.”

Walioyasikia haya wakapendekezwa sana na uelewa na akili yake. Kisa hiki ni sahihi sana.

[1] Muslim (2956), at-Tirmidhiy (2426), Ibn Maajah (4113) na Ahmad (2/323).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 131-132
  • Imechapishwa: 18/03/2017