36. Du´aa kwa mnasaba wa mgeni


151- ´Abdullaah bin Busr (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimkaribisha baba yangu. Tukamkaribisha chakula na Watbah[1] na akakila. Kisha akaletewa tende. Akazila na akakusanya kokwa baina ya kidole cha shahaadah na kidole cha katikati. Kisha akaletewa kinywaji na akanywa. Halafu akampa ambaye alikuwa kuliani mwake. Baada ya hapo baba yangu akachukua hatamu ya mnyama wake na kusema: ”Tuombee kwa Allaah.” Hivyo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

اللهُمَّ بَارِك لهم فيما رَزَقْتهم واغْفِرْ لَهُمْ وارْحَمْهُمْ

“Ee Allaah! Wabariki katika ulichowaruzuku, uwasamehe na uwarehemu.”

152- Anas (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimkaribisha Sa´d bin ´Ubaadah. Akamkaribisha kwa kumpa mkate na mafuta. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akala kisha baada ya hapo akasema:

أَفْطرَ عِنْدَكُم الصَّائِمُونَ وَأَكَلَ طَعَامَكُمْ الأَبْرَارُ وَصَلَّتْ عَلَيْكُم الملائِكَةُ

”Wafuturu kwenu waliofunga. Wale chakula chenu waliowema. Malaika wakuswalieni.”

[1] Aina ya chakula cha kusagwa kama viazi mviringo kilichochangwa na tende, jibini na mafuta.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 99-100
  • Imechapishwa: 21/03/2017