36. Dalili za kiakili juu ya kuthibiti kwa majina na sifa za Allaah

Dalili za kiakili juu ya kuthibiti kwa majina na sifa za Allaah zilizothibitishwa na Shari´ah ni kwa kusema:

1- Viumbe hivi vikubwa pamoja na sampuli zake, kutofautiana kwavyo na mpangilio wake juu ya kutekeleza manufaa yake na kupita juu ya zile njia walizowekewa ni mambo yanayofahamisha juu ya utukufu, uwezo, elimu, hekima, matakwa na utashi wa Allaah.

2- Kuneemeka, kufanyiana wema, kuondosha madhara na kuondosha matatizo; mambo haya yanafahamisha juu ya rehema, ukarimu na utoaji.

3- Adhabu na kuwapatiliza watenda madhambi yanathibitisha kwamba Allaah amewakasirikia na anawachukia.

4- Kuwakirimu wafanyao wema na kuwalipa thawabu yanathibitisha kwamba Allaah amewaridhia na anawapenda.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 67
  • Imechapishwa: 02/03/2020