36. Dalili ya thelathini na nne kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


34- Muhammad ametukhabarisha: Ahmad bin al-Hasan bin Khayruun ametuhadithia: Abul-Qaasim bin Bishraan ametuhadithia: Abu ´Aliy Ahmad bin al-Fadhwl bin al-´Abbaas bin Khuzaymah ametuhadithia: ´Aliy bin al-Husayn bin Yaziyd as-Suddaa-iy ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia: al-Waliyd bin al-Qaasim ametuhadithia, kutoka kwa Yaziyd bin Kaysaan, kutoka kwa Abu Haazim, kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna mja mwenye kusema “Hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah” kwa moyo msafi, isipokuwa inapanda na hairudishwi na kizuizi. Inapofika kwa Allaah basi Anamtazama yule aliyeisema. Ni haki ya Allaah kumtomtazama mpwekeshaji isipokuwa anamrehemu.”[1]

[1] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy aliyesema:

”al-Khatwiyb amemtaja ´Aliy bin al-Husayn bin Yaziyd as-Swuddaa-iy katika ”Taariykh Baghdaad” (11/394) na akasema kuwa alifariki mwaka wa 386. Halafu hakutaja kama amejeruhiwa au kusifiwa… Imaam at-Tirmidhiy ameipokea Hadiyth kwa njia nyingine kupitia kwa al-Husayn bin Yaziyd:

“Hakuna mja mwenye kusema “Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah” kwa moyo msafi, isipokuwa anafunguliwa milango ya Pepo mpaka inafika katika ´Arshi – midhali ni mwenye kujiepusha na dhambi kubwa.” (at-Tirmidhiy (3590))

Hii inathibitisha kwamba naona kuwa ´Aliy bin al-Husayn ni dhaifu kwa vile anakwenda kinyume na muundo wa at-Tirmidhiy pamoja vilevile anasimulia Hadiyth chache. Kwa ajili hiyo ndio maana nimetaja muundo wa at-Tirmidhiy katika ”Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah” na ”al-Mishkaat” (2314).” (Silsilat-ul-Ahaadiyth adh-Dhwa´iyfah” (2/320))

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 127-128
  • Imechapishwa: 12/06/2018