36. Dalili ya kwamba maneno ya Allaah hayakuumbwa

36- Ahmad bin Muhammad bin Mansuur ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Muhammad ametuhadithia… ح Muhammad bin ´Abd bin ´Abdih ametuhadithia: al-Idriys ametuhadithia: Abuu Muslim ametuhadithia: Abuu ´Aaswim ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Rifaa´, kutoka kwa Suhayl… ح ´Abdul-´Aziyz bin al-Mukhtar ametuhadithia: Suhayl ametuhadithia… ح al-Qaadhwiy Abuu Mansuur ametuhadithia: Haaruun bin Ahmad ametuhadithia: ´Aliy bin al-´Abbaas al-Bujaaliy ametuhadithia: Ibraahiym bin Yuusuf al-Hadhwramiy ametuhadithia… ح Muhammad bin Ahmad al-Jaaruudiy ametuhadithia kwa kutusomea: Muhammad bin ´Abdillaah al-Quraashiy ametuhadithia: Muhammad bin Swaalih ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Bahraam al-Kilaaniy al-Kuufiy ametuhadithia: al-Ashja´iy ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan ath-Thawriy, kutoka kwa Suhayl bin Abiy Swaalih, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kusema wakati jua linapozama:

أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ الله التامَّاتِ من شَرِّ مَا خَلَقَ

“Najilinda na maneno ya Allaah yaliyokamilika kutokana na shari ya vile alivyoviumba.”

hatodhuriwa na kitu katika usiku huo.”[1]

[1] Muslim (2709) na Ahmad (2/375).

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 73
  • Imechapishwa: 12/02/2017