Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya hajj ni Kauli Yake (Ta´ala):

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ

”Kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo wa kuiendea. Na atakayekanusha, basi hakika Allaah ni mkwasi kwa walimwengu.” (Aal ´Imraan 03 : 97)

MAELEZO

Dalili ya hajj ni maneno Yake (Ta´ala):

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ

”Kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo wa kuiendea. Na atakayekanusha, basi hakika Allaah ni mkwasi kwa walimwengu.” (03:97)

Inatakiwa kutekelezwa angalau mara moja katika maisha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hajj inafanywa mara moja. Atakayezidisha basi hiyo ni sunnah.”[1]

Hizi ndio nguzo tano za Uislamu.

[1] Ahmad (01/255), Abu Daawuud (1721), an-Nasaa´iy (2619), Ibn Maajah (2886) na al-Haakim (1728). Swahiyh kwa mujibu wa al-Haakim na adh-Dhahabiy ameafikiana naye.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 42
  • Imechapishwa: 19/01/2017