36. Allaah hana mke wala mshirika

Vilevile Allaa hana wake. Vipi atakuwa na mtoto ilihali hana mke?

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُ صَاحِبَةٌ

“Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Iweje Awe na mwana na hali hana mke!”[1]

Yeye hamuhitajii kiumbe yeyote. Hana haja ya mtoto wala mtoto. Hana haja ya viumbe kabisa. Kwa sababu Yeye ni Tajiri na wao ni ndio wenye kumuhitajia Yeye.

Hana mshirika wa aina yoyote; hana mshirika inapokuja kwa mtoto, mke, majina na sifa. Hakuna yeyote anayefanana na kulingana Naye (Subhaanahu wa Ta´ala). Hana mshirika inapokuja katika dhati Yake, majina na sifa na ´ibaadah.

[1] 6:101

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 32
  • Imechapishwa: 19/07/2021