36. al-´Ayyaashiy upotoshaji wa tisa wa al-Baqarah


al-´Ayyaashiy amesema:

أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِن بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَـٰهَكَ وَإِلَـٰهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ

“Je, mlikuwa mashahidi wakati mauti yalipomfikia Ya’quwb alipowaambia wanawe: “Mtaabudu nini baada yangu?” Wakasema: “Tutamwabudu Mola Wako na Mola wa baba zako, Ibraahiym na Ismaa’iyl na Ishaaq; Mungu Mmoja, nasi Kwake tunajisalimisha.” (02:133)

“Jaabir ameeleza ya kwamba alimuuliza Abu Ja´faar kuhusiana na Aayah hii:

Amesema: “Inamuhusu al-Qaa´im.”[1]

Yuko wapi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Wako wapi Maswahabah? Yuko wapi ´Aliy? Iko wapi familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Wako wapi wana wa Ibraahiym wanaozungumzishwa? Allaah Amemtakasa Abu Ja´faar na uongo huu. Ninaapa kwa Allaah hakuwa anajua mambo yalofichikana na hakuzungumza kuhusu al-Qaa´im wala al-Qaa´id. Yeye mwenyewe hakuwa anajua yatayomfika kesho. Huyu al-Qaa´im si jengine isipokuwa ni uongo tu wa Raafidhwah ili waweze kula pesa za Raafidhwah wajinga kwa jina la khumus [1/5] ya uongo.

[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/61).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 70
  • Imechapishwa: 19/03/2017