35. Unasemaje juu ya wanafunzi ambao wameshughulishwa sana na Hizbiyyuun na wameacha kutafuta elimu?

Swali 35: Baadhi ya wanafunzi wachanga wamejishughulisha na Hizbiyyuun na muda wao karibu wote unaishia katika wao na badala yake wameacha mambo yenye kuwanufaisha mbele ya Mola wao na ambao wanabainisha mabaya kutokamana na mazuri mpaka yajulikane yale makosa walionayo Hizbiyyuun. Hamu yao kubwa imekuwa ni kuuliza “unasemaje juu ya huyu na yule” na vikao vyao vingi ni vyenye kuzungumzia haya.  Hali imefikia kiasi cha kwamba wanawatuhumu watu kwa dhuluma. Ni ipi nasaha yako kwa vijana hawa? Tunaomba uwanasihi kutulia umuhimu elimu ya dini ambayo itawasalimisha na Bid´ah.

Jibu: Uhakika wa mambo ni kuwa haifai kupindukia katika mambo haya ambayo yanamtoa mwanafunzi kutamka haki na badala yake akaenda katika mabishano na akapoteza wakati katika kuzungumza mambo ambayo hayamletei faida yoyote. Bali hatimae inakuwa mtu anazunguka katika halaka mbalimbali. Inatakikana kwa mwanafunzi kutumia wakati wake katika kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), kufanya tafiti za kielimu na kuhudhuria halaka mbalimbali. Ni sawa akasikiliza matahadharisho juu yao na mabainisho ya sifa zao ili aweze kutahadhari nao. Ni bila shaka ya kwamba ingelikuwa ni kosa kubwa kwetu lau tungejaalia wakati wote ni kuwazungumzia wao na kuacha kujishughulisha na kujifunza elimu yenye manufaa.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 23/07/2017