Shaytwaan alikuwa amejionyesha kwa Quraysh kwa sura ya Suraaqah bin Maalik Ja´sham. Suraaqah bin Maalik Ja´sham alikuwa mkuu Madlaj. Akajitolea kuwachangia na akawashaji´isha kutoka kwenda vitani. Quraysh walikuwa wakichelea Banuu Madlaj wasije kuchukua fursa na wakashambulia familia zao na mali zao. Ndipo Allaah (Ta´ala) akasema:

وَإِذْ زَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ وَقَالَ لَا غَالِبَ لَكُمُ الْيَوْمَ مِنَ النَّاسِ وَإِنِّي جَارٌ لَّكُمْ ۖ فَلَمَّا تَرَاءَتِ الْفِئَتَانِ نَكَصَ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ وَقَالَ إِنِّي بَرِيءٌ مِّنكُمْ إِنِّي أَرَىٰ مَا لَا تَرَوْنَ إِنِّي أَخَافُ اللَّـهَ ۚ وَاللَّـهُ شَدِيدُ الْعِقَابِ

“Wakati shaytwaan alipowapambia matendo yao na akasema: “Hakuna watu wa kukushindeni leo hii na mimi nimesimama upande wenu.” Vilipoonana vikosi viwili, alirejea nyuma kwa visigino vyake na akasema: “Hakika mimi nimejitoa dhima kabisia nanyi; hakika mimi naona msiyoyaona hakika mimi namkhofu Allaah – na Allaah ni Mkali wa kuadhibu.”[1]

Hayo ni kwa sababu aliwaona Malaika pindi walipoteremka kwa ajili ya mapambano. Aliona mambo ambayo hakuyaona hapo kabla na hatimaye akakimbia.

Malaika wakapigana kama ambavo Allaah alivyowaamrisha. Pindi mtu katika waislamu alipokuwa akimshambulia adui wake basi anaona namna anavyoanguka mbele yake. Allaah akawafanya waislamu kuwakunguka kwelikweli washirikina. Mtu wa kwanza katika washirikina aliyejaribu kukimbia alikuwa ni Khaalid bin al-A´lam ambapo akakamatwa mateka. Waislamu wakawafuata. Wakawaua na wakawashika mateka. Washirikina sabini wakauawa, sabini wengine wakashikwa mateka. Mali zao zikafanywa ngawira. Miongoni mwa jumla ya washirikina ambao waliuawa ni wale ambao aliwataja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku kabla yake akiwemo Abu Jahl (Abul-Hakam ´Amr bin Hishaam) (Allaah amlaani). Aliuawa na Mu´aadh bin ´Amr bin al-Jamuuh na Mu´awwidh bin ´Afraa´. Aliyemmalizia ni ´Abdullaah bin Mas´uud ambaye alikihifadhi kichwa chake na akamletea nacho Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akafurahishwa na hilo.

[1] 08:48

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 51
  • Imechapishwa: 09/10/2018