35. Jihaad ni yenye kuendelea mpaka siku ya Qiyaamah

Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Vita ni vyenye kuendelea pamoja na viongozi wema na waovu mpaka siku ya Qiyaamah na haitakiwi kuachwa.”

MAELEZO

Vita ni vyenye kuendelea pamoja na viongozi, bi maana watawala, na swalah ya ijumaa na swalah za ´iyd mbili ni wajibu kwa kila yule ambaye yuko chini yake. Ni lazima kwao kupigana bega kwa bega pamoja naye dhidi ya makafiri na waasi. Hayo yameamrishwa na Allaah (´Azza wa Jall) pale aliposema:

وَإِن طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا ۖ فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَىٰ فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ

“Ikiwa makundi mawili ya waumini yatapigana, basi suluhisheni kati yao. Endapo mojawapo likikandamiza jengine, basi piganeni na ambalo linakandamiza mpaka lielemee katika amri ya Allaah.”[1]

Kiongozi ambaye uongozi wake umekubaliwa na waislamu – ni mamoja ameupata kwa mashauriano au kimabavu – ni lazima atiiwe. Ni lazima vilevile kupambana chini ya uongozi wake. Yule mwenye kufanya upungufu katika hayo basi ataulizwa mbele ya Allaah, kwa sababu ameacha jambo la wajibu.

[1] 49:09

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 138
  • Imechapishwa: 29/04/2019