35. Idadi ya chini ya kufaa kusimamisha swalah ya ijumaa

Swali 35: Nimesoma katika baadhi ya vitabu kwamba miongoni mwa sharti za kusimamisha swalah ya ijumaa ni kupatikane watu arobaini miongoni mwa wale watu ambao swalah inawawajibikia. Kumetangulia kuenezwa fatwa katika “ad-Da´wah” ya wewe muheshimiwa ya kwamba inaswaliwa kwa watu wawili pamoja na imamu. Ni vipi tutaoanisha kati ya mambo haya mawili[1]?

Jibu: Kushurutisha watu arobaini kwa ajili ya kusimamisha swalah ya ijumaa ni maoni yamesemwa na kikosi cha wanazuoni. Mmoja wao ni Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah). Maoni yenye nguvu ni kufaa kuisimamisha kwa idadi ya watu chini ya arobaini. Idadi ya lazima ni ya watatu kama ilivyotangulia katika fatwa nilipokuwa najibu swali kabla ya hili. Kwani hakuna dalili juu ya kushurutisha watu arobaini. Hadiyth iliopokelewa inayoshurutisha watu arobaini ni dhaifu. Hayo yamewekwa wazi na Haafidhw Ibn Hajar katika “Buluugh-ul-Maraam”.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/327).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 74
  • Imechapishwa: 03/12/2021