35. Du´aa wakati wa chakula na kunywa


Allaah (Ta´ala) Amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّـهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ

Enyi mlioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni na mshukuruni Allaah mkiwa mnamwabudu Yeye Pekee.” (al-Baqarah 02: 172)

143- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ewe mwanangu! Taja jina la Allaah. Kula kwa mkono wako wa kulia na kula vilivyo karibu nawe.”

144- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mmoja wenu akila ataje jina la Allaah (Ta´ala) mwanzoni. Akisahau kutaja jina la Allaah (Ta´ala) mwanzoni aseme:

بسْمِ اللهِ أَوَّله وَآخِره

”Kwa jina la Allaah; mwanzoni na mwishoni wake.”

145- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa kamwe hakitii kasoro chakula. Akikipenda, anakula. La sivyo anakiacha.”

146- Wahshiy ameeleza kwamba Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wamesema:

”Ee Mtume wa Allaah! Tunakula pasina kushiba.” Akasema: ”Huenda mnafarakana?” Wakasema: ”Ndio.” Hivyo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Kusanyikeni katika chakula chenu na tajeni jina la Allaah. Kitawabarikini.”

147- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah Humridhia mja ambaye anamhimidi Allaah baada ya kila chakula anachokula na kila kinywaji anachokunywa.”

148- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Anayekula chakula na kusema:

الْحَمْدُ للهِ الَّذي أَطْعَمَني هذَا الطَّعَام وَرَزَقَنيهِ مِنْ غَيْرِ حَوْلٍ مني وَلاَ قُوَّةٍ

“Himdi zote ni Zake Allaah ambaye amenilisha mimi [chakula] hichi na akaniruzuku pasina uwezo wangu wala nguvu zangu.”

madhambi yake yaliyotangulia hufutwa.”

149- Kuna mtu ambaye alikuwa akimhudumia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kwamba alikuwa akimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi anapoletewa chakula husema:

بسْمِ اللهِ

”Kwa jina la Allaah.”

Wakati anapomaliza kula husema:

اللَّهُمَّ أَطْعَمْتَ وَأَسْقَيْتَ وَأَغْنَيْتَ وَأَقْنَيْتَ وَهَدَيْت وَاجْتَبَيْتَ لَكَ الْحَمْدُ على مَا أَعطَيْتَ

”Ee Allaah! Umelisha na kunywisha, kutajirisha, kukinaisha, kuongoza na kubuni. Ni Zako himdi zote kwa ulichokitoa.”

150- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati chakula chake kinapotengwa alikuwa akisema:

الْحمد لله كَثيراً طَيِّباً مباركاً فيه غَيْرَ مَكْفِيٍّ وَلاَ مُوَدَّع وَلا مُسْتَغْنىً عَنْه رَبَّنَا

“Himdi zote ni Zake Allaah, zilizo nzuri, zenye baraka, zisizotoshelezwa wala kuagwa, wala kutoshwa nazo mtu. Ee Mola wetu.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 96-99
  • Imechapishwa: 21/03/2017