35. Dalili ya thelathini na tatu kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

33- Twaahir bin Muhammad al-Maqdisiy ametukhabarisha: Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: al-Qaasim bin Abiyl-Mundhir ametuhadithia: ´Aliy bin Ibraahiym bin Salamah ametuhadithia: Muhammad bin Yaziyd ametuhadithia: Bakr bin Khalaf ametuhadithia: Yahyaa bin Sa´iyd alinihadithia, kutoka kwa Muusa bin Abiy ´Iysaa at-Twahhaan, kutoka kwa ´Awn bin ´Abdillaah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa nduguye, kutoka kwa an-Nu´maan bin Bashiyr  ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Miongoni mwa matamshi yenu ya kumtukuza Allaah ni pamoja na “Tasbiyh, Tahliyl na Tahmiyd. Vimeizunguka ´Arshi, yanatoa sauti kama bin na kumtaja yule mwenye kuyatamka. Hapendi mmoja wenu atajwe kwa ajili ya hilo?”[1]

[1] Ibn Maajah (3809) na al-Haakim (1/503) ambaye amesema:

”Hadiyth iko kwa mujibu wa masharti ya Muslim.”

Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (3086).

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 127
  • Imechapishwa: 12/06/2018