Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya swawm ni Kauli Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa swawm kama ilivyoandikwa kwa walio kabla yenu – ili mumche.” (al-Baqarah 02:183)

MAELEZO

Dalili inaendelea mpaka katika maneno Yake (Subhaanah):

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

“Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa ndani yake Qur-aan ili iwe ni mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na upambanuo wa haki na batili. Basi katika nyinyi atakayeshuhudia [kuandama kwa] mwezi na afunge. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini basi [atimize] idadi katika siku nyinginezo. Allaah anakutakieni mepesi na wala hakutakieni magumu. [Fungeni] ili mkamilishe idadi na ili mumkabiri Allaah kwa kuwa amekuongozeni na ili mpate kushukuru.” (02:185)

Bi maana kufunga ni wajibu kwenu katika Ramadhaan ya kila mwaka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 42
  • Imechapishwa: 17/01/2017