35. Dalili juu ya kucheka kwa Allaah 3


34- Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia: Rawh ametuhadithia: Ibn Jurayj ametuhadithia, kutoka kwa Abuz-Zubayr aliyesimulia kuwa amemsikia Jaabir akiulizwa kuhusu Swiraat. Akataja Hadiyth ambapo akasema:

Allaah (´Azza wa Jal) atasema: “Mimi ni Mola wenu.” Watasema: “Mpaka tukuone kwanza.” Ndipo Ajifunue kwao hali akicheka.”

Amesema: “Nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema hivo.”[1]

Ameipokea Muslim katika mlango unaozungumzia imani kupitia kwa ´Ubaydullaah na Ishaaq bin Mansuur, kutoka kwa Rawh, kutoka kwa ´Ubaadah, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Jaabir.

[1] Muslim (191) na Ahmad (3/383).

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 74-75
  • Imechapishwa: 02/03/2018