35. al-´Ayyaashiy upotoshaji wa nane wa al-Baqarah

al-´Ayyaashiy amesema wakati alipokuwa anafasiri Aayah:

رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ

“Mola wetu! Tujaalie tuwe Waislamu [wenye kujisalimisha] Kwako pamoja na kizazi chetu kiwe ni chenye kujisalimisha Kwako. Tufunze taratibu za kutekeleza ‘ibaadah zetu na Pokea tawbah zetu; hakika Wewe ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu!” (02:128)

“Abu ´Amr az-Zubayriy amepokea ya kwamba alimuuliza Abu ´Abdillaah: “Ni wepi Ummah wa Muhammad?” Akasema: “Ni Banuu Haashim peke yake.” Akasema: “Iko wapi dalili juu ya kwamba Ummah ni watu wa familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tu pasina wengine?” Akasema: “Kauli ya Allaah:

رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ

“Mola wetu! Tujaalie tuwe Waislamu [wenye kujisalimisha] Kwako pamoja na kizazi chetu kiwe ni chenye kujisalimisha Kwako. Tufunze taratibu za kutekeleza ‘ibaadah zetu na Pokea tawbah zetu; hakika Wewe ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu!”[1]

Halafu akaendelea kumsemea uongo Allaah na Abu ´Abdillaah. Lengo ni kuutoa Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Uislamu na khaswa Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na Maswahabah watukufu wengine waliobaki (Radhiya Allaahu ´anhum) katika Muhaajiruun na Answaar ambao Allaah Amewaridhia.

Je, ametambua kuwa amejitoa yeye mwenyewe na Raafidhwah katika Uislamu pasina kujua hilo? Je, ametambua kuwa amekanusha ujumbe wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa walimwengu wote pasina kujua hilo?

[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/60-61).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 69
  • Imechapishwa: 19/03/2017