34. Vipi kutangamana na walinganizi Salafiyyah wenye kuchanganyika na Ahl-ul-Bid´ah?

Swali 34: Mjuzi anayewatambua Ahl-ul-Bid´ah anaweza kutahadharisha juu yao. Lakini kuna Ahl-ul-Hadiyth wanaochanganyika na Ahl-ul-Bid´ah mpaka kitendo hichi kinapelekea kuwadanganya wale wasiokuwa wasomi. Vipi mtu afanye nini juu ya hili?

Jibu: Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba watu wanatofautiana. Lakini mara nyingi kila ambaye anaficha jambo lake ni lazima Allaah alifichue kwa njia hii au ile. Mtu ambaye anawadhihirishia watu kuwa yuko juu ya Sunnah na Salafiyyah, ilihali ni mzushi, ni lazima Allaah amfichue vovyote iwavyo. Ni lazima aoneshe mambo fulani yenye kufahamisha kile alichomo katika Bid´ah. Akionesha kitu katika Bid´ah basi ni lazima atahadharishwe. Ama endapo hadhihirishi kitu, basi hakuna nguvu wala njia isipokuwa kwa msaada wa Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 23/07/2017