34. Sura ya kwanza: Dalili kutoka katika Qur-aan, Sunnah na akili juu ya kuthibiti kwa majina na sifa za Allaah

3- Ndani yake kuna yafuatayo:

Sura ya kwanza: Dalili kutoka katika Qur-aan, Sunnah na akili juu ya kuthibiti kwa majina na sifa za Allaah.

Sura ya pili: Mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kuhusu majina na sifa za Allaah.

Sura ya tatu: Radd kwa mwenye kupinga majina na sifa au akapinga kitu katika hayo.

1- Sura ya kwanza: Dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah

Tumeshatangulia kutaja kwamba Tawhiyd imegawanyika aina tatu: Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah, Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah na Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swiffaat. Vilevile tumeshataja jumla ya aina mbili za mwanzo ambazo ni Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Hivi sasa tunataja dalili ya sampuli hii ya mwisho: Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swiffaat. Hapa tutakutajia baadhi ya dalili za Qur-aan. Maneno Yake (Ta´ala):

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ

”Allaah ana majina mazuri mno, hivyo basi muombeni kwayo na waacheni wale wenye kupondoka katika kuyapotosha majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda.”[1]

Allaah (Subhaanah) katika Aayah hii amejithibitishia majina, akaeleza kwamba ni mazuri mno na akaamrisha kumuomba kwayo kwa kusema:

“Ee Allaah! Mwingi wa huruma! Mwenye kurehemu! Mwenye kusimamia kila kitu! Mola wa walimwengu!”

Amewatishia wale ambao wanayaharibu majina Yake. Kuharibu bi maana wanayapondosha kutokamana na haki ima kwa kumkanushia nayo Allaah, kuyapindisha kinyume na maana yake sahihi au aina nyenginezo za aina ya kuyaharibu. Amewatishia kwamba atawalipa kwa vitendo vyao viovu. Amesema (Ta´ala):

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ

“Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye, anayo majina mazuri mno.”[2]

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ

”Yeye ni Allaah, ambaye hakuna mungu wa haki isipokuwa Yeye, mjuzi wa yaliyofichikana na ya dhahiri, Yeye ni Mwenye kurehemu. Yeye ni Allaah, ambaye hakuna mungu wa haki isipokuwa Yeye, mfalme, mtakatifu, Mwenye kusalimisha na kusalimika, Mwenye kusadikisha ahadi na kuaminisha, Mwenye kudhibiti, kushuhudia, kuchunga na kuhifadhi, Mwenye nguvu zisizoshindwa, Jabari, Mwenye ukubwa na utukufu – Utakasifu ni wa Allaah kutokamana na ambayo wanamshirikisha. Yeye ni Allaah, muumbaji, mwanzishi viumbe, muundaji sura – ana majina mazuri mno. Kinamtukuza kila kilichokuweko katika mbingu na ardhi Naye ni Mwenye nguvu zisizoshindwa, Mwenye hekima.”[3]

Aayah hizi zimefahamisha Allaah kuwa na majina.

[1] 07:180

[2] 20:08

[3] 59:22-24

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 64-65
  • Imechapishwa: 27/02/2020