34. Qur-aan na Sunnah inampa faraja kila mwenye zito na dhiki

Yule mwenye kuacha Qur-aan na Sunnah vikahukumu basi atamfanyia faraja kila jambo lake zito na njia ya kutokea kwa kila dhiki yake.

Miongoni mwa mambo ambayo wale wanaowakaripia wale watawala wanaohukumu kwa sheria zilizotungwa na wanadamu wanatakiwa kuhisi ni kwamba wao pia wanahukumu kwa Shari´ah isiyokuwa ya Allaah katika miamala na mambo yao. Simaanishi kuwa wanahukumu kinyume na Shari´ah ya Allaah (´Azza wa Jall) katika mambo yote hayo. Lakini nitakuwa si mwenye kuongeza chumvi nikisema kuwa wanafanya hivo katika mambo yao mengi.

Kwa hiyo wanatakiwa kumcha Allaah juu ya nafsi zao na wanapaswa kuzifanyia hesabu nafsi zao kabla hawajafanyiwa.

Mafanikio yote ni kwa msaada wa Allaah. Swalah, salamu na baraka zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 80-81
  • Imechapishwa: 19/11/2020