34. Ni ipi hukumu ya kukesha usiku kutwa katika michezo?

Swali 34: Ni ipi hukumu ya kukesha usiku wa Ramadhaan na kucheza?

Jibu: Ni kupoteza wakati. ´Ibaadah ni mtu kuutumia usiku kwa kuswali, kusoma Qur-aan na kusoma elimu. Watu hawa wanapoteza usiku katika mipira na michezo. Hii bila ya shaka ni kupoteza wakati. Kisha wanautumia mchana kutwa na wanaamka karibu na kuzama kwa jua. Huenda hawaswali Fajr, Dhuhr na ´Aswr. Hii ni dhambi kubwa!

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 47-48
  • Imechapishwa: 12/06/2017