34. Mwenye busara na mpumbavu II


1 – Baadhi ya sifa za mpumbavu ni haraka, kutokuwa na uoni wa mbali, kushindwa, madhambi, ujinga, chuki, udhaifu, majitapo, hasadi, khiyana, ughafilikaji, usahaulifu, upotofu, machafu, majivuno, unyanyaso na bughudha.

2 – Moja katika alama kubwa kwa mpumbavu ni ulimi wake. Moyo wake unakuwa kwenye ncha ya ulimi wake. Kinachokuja katika moyo wake ndicho kinachotamkwa na ulimi wake.

3 – Ni wajibu kwa mwenye busara kumuepuka mtu aliye na sifa hizi. Watu hawa wanawavamia wale wanaoishi nao. Huwaoni Zuttw[1] sio mashujaa ya watu. Lakini hata hivyo wanathubutu kwa simba kwa sababu ya ule wingi wa kuwaona.

4 – Wahb bin Munabbih amesema:

“Mpumbavu ni kama nguo iliochanikachanika. Ukitia kiraka upande mmoja inachanika upande mwingine. Ni kama mfano wa chombo cha udongo kilichovunjika. Hakiwezi kutengenezwa wala kurudishwa kufanywa udongo.”

5 – Ukitangamana na mpumbavu, basi utaudhika. Ukimtenga, anakutukana. Akikupa, atakukumbusha alichokufanyia. Ukimpa, si mwenye shukurani. Akikueleza siri, anakushakia. Ukimueleza siri, anakukhini. Akiwa juu yako, basi anakudharau. Akiwa chini yako, basi anakutukana.

6 – Mpumbavu hudhani kuwa yeye ndiye kiumbe aliye na akili zaidi na viumbe wengine wote ni wapumbavu. Mpumbavu ndiye mtu anayechukiliwi zaidi na watu. Hajulikani duniani. Matendo si yenye kuridhiwa. Si mwenye kusifiwa mbele ya Allaah na kwa watu wema.

7 – al-Hasan amesema:

“Mimi ni mwenye matarajio zaidi kwa aliye na subira ambaye amenipa mgogno kuliko mpumbavu anayenijia.”

8 – Ni wajibu kwa mwenye busara asitangamane kabisa na ambaye hanufaiki kutoka kwake.

9 – Miongoni mwa sifa za mwenye busara ni upole, ukimya, utulivu, utimilifu, kujitolea, hekima, elimu, kujichunga, uadilifu, nguvu, maamuzi, akili, upambanuzi, kujishusha chini, kupuuzilia mbali, kushusha macho chini, kujichunga na machafu na kuwatendea wengine yaliyo mema. Mtu akijaaliwa kutangamana na mtu mwenye busara basi amshike mkono na kamwe asimwache.

10 – Maalik bin Diynaar amesema:

“Mtawa mmoja aliyekuweko ndani ya seli yake alinambia: “Nakutahadharisha na kila tangamano ambalo hunufaiki kwalo jema lolote. Usiketi naye si kwa karibu au kwa mbali.”

[1] ”Aina fulani ya weusi na wahindi walio na miili mirefu na miembamba.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 121-124
  • Imechapishwa: 02/08/2021