Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

32- Kila kitu kinapitika kwa makadirio na utashi Wake.

MAELEZO

Hapana shaka kwamba kila kitu kinapitika kutokana na makadirio Yake. Hakuna chochote kinachotoka nje ya makadirio Yake; si kheri, si shari, utiifu, maasi, kufuru, imani, maradhi, afya njema, utajiri, umasikini, elimu na ujinga. Kila kitu kinatokea kwa makadirio Yake. Hakuna chochote katika ufalme Wake kinachotokea mbali na kile alichokikadiria na kukitaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 50
  • Imechapishwa: 25/09/2019