34. ´Ibaadah ni kwa ajili ya Allaah pekee


Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا

“Na kwamba misikiti yote ni ya Allaah, hivyo basi msiombe yeyote pamoja na Allaah!” (al-Jinn 72 : 18)

Mwenye kumtekelezea chochote katika hayo mwengine asiyekuwa Allaah ni mshirikina kafiri. Dalili ya hilo ni Kauli Yake (Ta´ala):

وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚإِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ

“Yeyote yule anayeomba pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wowote juu ya hilo, basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake, kwani hakika hawafaulu makafiri.” (al-Mu´minuun 23 : 117)

MAELEZO

Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) ametaja baadhi ya aina za ´ibaadah. Halafu akataja kwamba yule mwenye kumtekelezea yoyote katika hizo asiyekuwa Allaah kwamba ni mshirikina na kafiri. Ametumia dalili maneno Yake (Ta´ala):

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا

“Na kwamba misikiti yote ni ya Allaah, hivyo basi msiombe yeyote pamoja na Allaah!”

وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚإِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ

“Yeyote yule anayeomba pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wowote juu ya hilo, basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake, kwani hakika hawafaulu makafiri.”

Dalili katika Aayah ya kwanza ni kwamba Allaah (Ta´ala) ameeleza kuwa misikiti, ambayo ni pale mahali pa kusujudia, au vile viungo vya kusujudia, ni ya Allaah. Akafuatishia hayo kwa kusema:

فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا

“Hivyo basi msiombe yeyote pamoja na Allaah!”

Bi maana msimwombe mwengine pamoja Naye ambapo mkamsujudia mwengine asiyekuwa Yeye.

Dalili katika Aayah ya pili ni kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amebainisha kuwa yule mwenye kumuomba mungu mwingine pamoja na Allaah kwamba ni kafiri. Amesema:

ۚإِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ

“Kwani hakika hawafaulu makafiri.”

Katika maneno Yake:

لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ

“… hana ushahidi wowote juu ya hilo… “

kuna ishara kwamba haiyumkiniki kukawa na ushahidi juu ya uwepo wa waungu wengi. Sifa “hana ushahidi wowote juu ya hilo” ni sifa ya kubainisha uhalisia wa mambo, na sio sifa ya kufungamanisha, inayopambanua mambo, kwa sababu haiwezekani kukawepo ushahidi juu ya kwamba kuna waungu wengine wanaoshirikiana pamoja na Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 54-55
  • Imechapishwa: 22/05/2020