34. Hakuna yeyote anayeshabihiana wala kulingana na Allaah


Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Hana anayeshabihiana Naye, hana anayelingana Naye, hana mtoto, hana wazazi, hana mke wala mshirika.

MAELEZO

Kama ambavo hakuna yeyote anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah (´Azza wa Jall) na kwamba vyote vinavyoabudiwa badala yake ni batili, basi vivyo hivyo hana yeyote anayeshabihiana Naye wala hana yeyote anayelingana Naye ambapo akapimwa au akasawazishwa Naye. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[1]

فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ

”Basi msimpigie mifano Allaah.”[2]

Ambapo mkamfananisha na wengine. Vilevile amesema:

هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا

“Je, unamjua yeyote mwenye jina kama Lake?”[3]

Mwitwaji jina ni mwenza. Bi maana hakuna anayeshabihiana Naye na wala hutambui yeyote ambaye anastahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye peke yake.

[1] 42:11

[2][2] 16:74

[3] 19:65

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 31
  • Imechapishwa: 19/07/2021