34. Dalili ya kwamba waumini watamuona Allaah Peponi

34- al-Haakim Muhammad bin Muhammad bin ´Abdillaah al-Azdiy ametuhadithia: Abuu Ishaaq al-Qarraab ametuhadithia: Abuu Ya´laa ametuhadithia: Hawtharah bin Ashras ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa Thaabit al-Bunaaniy, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa, kutoka kwa Suhayb (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu ya maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ

“Kwa wale waliofanya wema watapata mema zaidi na ziada.” (10:26)

“Mema zaidi ni Pepo na ziada ni kutazama uso wa Allaah (´Azza wa Jall).”[1]

[1] Ahmad (4/332), Muslim (181) na at-Tirmidhiy (2558).

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 73
  • Imechapishwa: 10/02/2017