34. Dalili juu ya kucheka kwa Allaah 2

33- Yahyaa bin Muhammad bin Swaa´id  ametuhadithia: Muhammad bin Haaruun Abu Nashiytw ametuhadithia: al-Mughiyrah ´Abdul-Qudduus bin al-Hajjaaj ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Yaziyd bin Tamiym ametuhadithia, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka wa Sa´iyd bin al-Musayyab, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyeeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wetu (´Azza wa Jall) anawacheka watu wawili. Mmoja kamuua mwenzake na wote wawili wakaingia Peponi.”[1]

´Abdur-Rahmaan amesema:

“az-Zuhriy aliulizwa juu ya tafsiri ya hii. Akasema: “Mshirikina kamuua muislamu, kisha akaingia katika Uislamu ambapo akafa na kuingia Peponi.”

[1] al-Bukhaariy (2826), Muslim (1890) na Ibn Maajah (191).

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 73-74
  • Imechapishwa: 02/03/2018