167- Kukusudia kwenda kutembea Yerusalemu baada ya kuhiji na kusema:

قدس الله حجتك

“Allaah aitakase hajj yako.”

168- Kutufu kwenye msikiti wa mwamba kama ambavyo watu wanavyotufu kwenye Ka´bah.

169- Kuadhimisha mwamba kwa aina yoyote ile ya maadhimisho. Kwa mfano kulipapasapapasa, kulibusu, kuwapeleka kondoo hapo ili kuwachinjia hapo, kujenga juu yake na mfano wake.

170- Kuna ambao wanadai kwamba kwenye mwamba mtu anaweza kuona athari ya miguu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na athari ya kilemba chake. Wako ambao wanadhani kwamba ndio mahali ambapo Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) anaweka mguu Wake.

171- Kutembelea sehemu ambayo wanadai ndiko kazaliwa ´Iysaa (´alayhis-Salaam).

172- Wanadai kwamba huko ndiko kuna Njia na Mizani. Wanasema pia kwamba njia itayotofautisha baina ya Pepo na Moto ni ukuta huo uliojengwa mashariki mwa msikiti.

173- Kuadhimisha mnyororo na sehemu zake.

174- Kuswali kwenye kaburi la Ibraahiym (´alayhis-Salaam).

175- Kukusanyika katika msimu wa hajj katika msikiti wa Aqswaa´ ili kuimba nyimbo na kupiga dufu.

Haya ndio ya mwisho niliyoweza kukusanya katika Bid´ah za hajj na matembezi yake. Ninamuomba Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ayajaalie kuwa ni yenye kuwasaidia waislamu juu ya kumuiga bwana wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kutakasika kutokamana na mapungufu ni Kwako, ee Allaah, na himdi zote ni Zako. Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Nakuomba msamaha na kutubia Kwako.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 22/07/2018