34. al-´Ayyaashiy upotoshaji wa saba wa al-Baqarah

al-´Ayyaashiy amesema wakati alipokuwa anafasiri Aayah:

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَـٰذَا بَلَدًا آمِنًا وَارْزُقْ أَهْلَهُ مِنَ الثَّمَرَاتِ مَنْ آمَنَ مِنْهُم بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ قَالَ وَمَن كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُ قَلِيلًا ثُمَّ أَضْطَرُّهُ إِلَىٰ عَذَابِ النَّارِۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ

“Na Ibraahiym alipoomba: “Mola wangu, Ufanye mji huu kuwa wa amani na Waruzuku watu wake katika matunda – atakayemwamini Allaah miongoni mwao na Siku ya Mwisho”, Akasema: “Na atakayekufuru, Nitamstarehesha kidogo kisha Nitamsukumiza katika adhabu ya Moto; na ni pabaya paliyoje pahala pa kuishia”. (02:126)

“´Abdullaah bin Ghaalid amepokea kutoka kwa baba yake, kutoka kwa mtu, kutoka kwa ´Aliy bin al-Husayn ambaye amefasiri maneo ya Ibraahiym:

رَبِّ اجْعَلْ هَـٰذَا بَلَدًا آمِنًا وَارْزُقْ أَهْلَهُ مِنَ الثَّمَرَاتِ مَنْ آمَنَ مِنْهُم بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ

“Mola wangu, Ufanye mji huu kuwa wa amani na Waruzuku watu wake katika matunda – atakayemwamini Allaah miongoni mwao na Siku ya Mwisho.”

“Anamaanisha sisi, mawalii Wake na kundi Lake na mteuliwa Wake[1]. Ndipo Aliposema:

وَمَن كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُ قَلِيلًا ثُمَّ أَضْطَرُّهُ إِلَىٰ عَذَابِ النَّارِۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ

“Na atakayekufuru, Nitamstarehesha kidogo kisha Nitamsukumiza katika adhabu ya Moto; na ni pabaya paliyoje pahala pa kuishia”.

Anamaanisha wale waliomkanusha mteuliwa Wake na wale katika Ummah wake wasiyomfuata. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba hali ya Ummah iko namna hii.”[2]

Hivi ndivyo wanafunzi wa Ibn Sabaa´ walivyoshikamana na Qur-aan. Namna hii ndivyo wanavyomtia sura Ibraahiym. Alikuwa hajali yeyote Shiy´ah na khaswa ikiwa ni katika waajemi!?!?

Ama inapokuja katika Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam, wote wamehukumiwa kufuru tokea wakati wa Muhammad!?!? Ni kwa vile Ummah hauna I´tiqaad ya Ibn Sabaa´. Kwani Ummah hauna I´tiqaad ya kizazi cha uyahudi.

[1] Bi maana ´Aliy

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/59).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 69
  • Imechapishwa: 19/03/2017