3- Jambo la kutendea kazi mema lisipelekee katika maovu ambayo ni makubwa zaidi kuliko manufaa yanayopatikana katika kutendea kazi mema hayo. Hali ikiwa ni hivo basi itambulike kuwa kuyazuia madhara kunatangulizwa kabla ya kuleta manufuaa. Msemo huu, ambao ni kanuni, wenye kufahamishwa na Qur-aan sio kwa njia ya moja kwa moja. Kwa msemo mwingine tunachotaka kusema ni kwamba si katika hali zote kuzuia kila dhara ni bora kuliko kufanya manufaa. Manufaa na madhara yakilingana basi lililo bora ni kuyazuia madhara. Madhara yakiwa makubwa zaidi kuliko manufaa lililo bora ni kuyazuia madhara. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ فَيَسُبُّوا اللَّـهَ عَدْوًا بِغَيْرِ عِلْمٍ

“Na wala msiwatukane wale wanaowaomba badala ya Allaah wasije nao kumtukana Allaah kwa uadui bila ya elimu.”[1]

Kila mmoja anajua kwamba kuwatukana waungu wa washirikina ni jambo lenye manufaa na ndani yake kuna kheri. Lakini manufaa haya yakipelekea katika maovu makubwa zaidi basi mtu anatakiwa mtu anatakiwa kuacha kufanya hivo. Kwa sababu sisi tukiwatukana waungu wao (na sisi tunafanya hivo kwa haki) basi jambo hilo litasababisha kutukanwa Allaah bila ya elimu. Inatakiwa kuzingatia nukta hii wakati wa kuamrisha mema na kukataza maovu.

Lakini ikiwa madhara yanamezwa zaidi upande wa manufaa basi tunayapa kipaumbele manufaa na wala hatujali [hayo madhara]. Hukumu nyingi za Kishari´ah na za kilimwengu ziko namna hii. Kwa mfano mvua hii inayonyesha na ndani yake kuna manufaa kwa jumla. Lakini ndani kuna madhara kwa mtu ambaye ndio punde amemaliza kujenga paa ya nyumba yake na mvua iliponyesha ikaiharibu. Hata hivyo madhara haya madogo ni yenye kumezwa na upande wa manufaa ambayo ni ya wengi. Vivyo hivyo hukumu za Kishari´ah kama za kilimwengu. Hili ni jambo ambalo mtu anatakiwa kutanabahi nalo. Huenda wakati mwingine sio katika maslahi kwetu kukataza maovu fulani kwa sababu yanapelekea katika madhara makubwa zaidi. Tunachofanya ni sisi kusubiri mpaka yakamilike mambo. Kwa ajili hii Shari´ah ya Kiislamu imekuja hatua kwa hatua katika kuweka Shari´ah ili watu waikubali polepole. Vivyo hivyo inapohusiana na maovu tunapaswa kuwatibu watu hadi mambo yatimie. Mambo yenyewe ni haya matatu:

1- Ujuzi wa hukumu.

2- Ujuzi wa hali.

3- Kufanya mema kusipelekee katika maovu ambayo ni makubwa zaidi kuliko manufaa.

[1] 06:108

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 44-46
  • Imechapishwa: 26/08/2019