6- ´Ibaadah imejengeka juu ya nguzo tatu ambazo ni:

1- Mapenzi.

2- Khofu.

3- Kutaraji.

Mapenzi pamoja na kujidhalilisha. Khofu pamoja na kutarajia. Ni lazima ´ibaadah ikusanye mambo haya. Allaah (Ta´ala) amesema alipowasifu waja Wake waumini:

يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ

“Atakaowapenda nao watampenda.”[1]

وَالَّذِينَ آمَنُواْ أَشَدُّ حُبًّا لِّلّهِ

“Lakini wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah.”[2]

Amesema tena katika kuwasifu Mitume na Manabii Wake:

إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ

“Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri na wakituomba kwa shauku na khofu na walikuwa wenye kutunyenyekea.”[3]

Baadhi ya Salaf wamesema:

“Mwenye kumwabudu Allaah kwa mapenzi peke yake ni mzandiki. Mwenye kumwabudu Allaah kwa kutaraji peke yake ni Murjiy. Mwenye kumwabudu kwa kuogopa peke yake ni Haruuriy[4]. Mwenye kumwabudu kwa mapenzi, khofu na kutaraji ni muumini na mpwekeshaji.”

Haya yamesemwa na Shaykh-ul-Islaam katika kitabu chake “al-´Ubuudiyyah”.

Vilevile amesema:

“Dini ya Allaah ni kumwabudu, kumtii na kumnyenyekea. Msingi wa ´ibaadah ni kujidhalilisha. Husemwa طريقٌ مُعبَّدٌ ikiwa imedhalilishwa na hukanyagwa kwa miguu. Lakini ´ibaadah iliyoamrishwa ndani yake kuna maana ya kujidhalilisha na maana ya kupenda. Ndani yake kuna upeo wa kujidhalilisha kwa Allaah (Ta´ala) na upeo wa kumpenda. Mwenye kumnyenyekea mtu pamoja na kumchukia hawi mja wake. Akikipenda kitu na asikinyenyekei hawi ni mja wacho. Ni kama ambavo mtu anampenda mtoto wake na rafiki yake. Kwa ajili hiyo hakitoshi kimoja wapo katika kumwabudu Allaah (Ta´ala). Bali ni lazima Allaah awe ni mwenye kupendwa zaidi kwa mja kuliko kila kitu na Allaah kwake awe ni mkubwa zaidi kuliko kila kitu. Bali hakuna anayestahiki mapenzi na unyenyekevu mkamilifu zaidi isipokuwa Allaah… “[5]

Hizi ndio nguzo za ´ibaadah ambazo inazunguka juu yake.

Yale ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameyawekea Shari´ah ndio inapozungukia ´ibaadah. ´Ibaadah haizungukii kwenye Bid´ah, mambo ya ukhurafi, matamanio na kuwafuata kichwa mchunga mababa.

[1] 05:54

[2] 02:165

[3] 21:90

[4] Bi maana ni katika Khawaarij.

[5] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/152).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 27/02/2020