33. Radd kwa wanaoifananisha mikono ya Allaah na ya viumbe


Kuhusu wafananishaji Qur-aan imewaraddi. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye.” (42:11)

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

“Na wala hakuna yeyote anayefanana na kulingana Naye.” (112:04)

هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا

“Je, unamjua mwengine anaye jina kama Lake?” (19:65)

فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Basi msimfanyie Allaah wenza na hali ya kuwa nyinyi mnajua.” (02:22)

Mwenza ni anayeshabihiana na kufanana Naye. Amekataza kumfanyia Allaah anaoshabihiana na kufanana Naye kutoka katika viumbe Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Hakuna kitu kinachofanana Naye.

Haya ndio madhehebu ya Jahmiyyah katika masuala ya mikono miwili ya Allaah (´Azza wa Jall). Wanaraddiwa namna hii vile walivyopindisha. Ndio madhehebu vilevile ya wafananishaji na wakanushaji na wanaraddiwa kupitia maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).