33. Qur-aan imeteremshwa kwa Muhammad ambapo akawafikishia Ummah wake

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Akayateremsha kwa mja na Mtume Wake na mwaminifu Wake juu ya Wahy Wake na balozi kati Yake na waja Wake; Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

MAELEZO

Akayateremsha kwa mja na Mtume Wake – Ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni mja na Mtume Wake.

Mja – Hapa kuna Radd juu ya wale wanaochupa mpaka kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanamfanya kuwa na kitu katika sifa za uungu. Yeye ni mja na sio mwabudiwa.

Mtume Wake – Hapa kuna Radd kwa wale wanaopinga ujumbe wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuna makundi mawili yanayogongana; kundi moja limechupa mpaka kwake na likamnyanyua katika ngazi ya uungu na kundi lingine limezembea katika haki yake na kupinga ujumbe wake. Sisi tunakiri yote mawili; kwamba ni mja na kwamba ni Mtume. Maneno yake:

“… mwaninifu Wake juu ya Wahy Wake.”

Ni mjumbe mwaminifu. Hakuzidisha ndani ya Qur-aan na wala hakupunguza. Bali ameifikisha kama ilivyokuja kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Amesema (Ta´ala):

وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِيلِ لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ

“Na lau kama angetutungia baadhi za kauli, bila shaka Tungelimchukua kwa mkono wa kuume.”[1]

Lau Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atasema juu ya Allaah na akamnasibishia ambayo hakusema basi Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) angelimwangamiza. Hapa kuna utakaso kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba amefikisha ufikishaji wa wazi. Yeye ni mfikishaji kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na ni mwaminifu juu ya Wahy. Kwa ajili hii siku moja wakati alipogawanya swadaqah na wakazungumza wenye kuzungumza katika wanafiki akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hivi kweli hamniamini ilihali naaminiwa na Yule aliye mbinguni?”[2]

Hamniamini juu ya kugawanya swadaqah ilihali naaminiwa na Yule aliye mbinguni – ambaye ni Allaah – juu ya Wahy?

Balozi kati Yake na waja Wake – Balozi ni Mtume. Mtume ndiye balozi kati ya Allaah na waja Wake katika kufikisha ujumbe. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amemtuma ili afikishe ujumbe wa Allaah.

[1] 69:44-45

[2] al-Bukhaariy (4351) na Muslim (1064) kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 54
  • Imechapishwa: 17/03/2021