3 – Kinachofanywa juu ya nywele za kichwani kwa mwanamke ambaye kishakufa. Zinafanywa mikia mitatu na inatupwa nyuma yake. Kutokana na Hadiyth ya Umm ´Atwiyyah juu ya namna ya kumuosha msichana wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Tukazifunga nywele zake mikia mitatu na tukazitupa nyuma yake.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

4 – Hukumu ya wanawake kulisindikiza jeneza. Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza:

“Tumekatazwa kufuata jeneza na wala hatukutiliwa mkazo.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Makatazo udhahiri wake ni uharamu. Maneno yake:

“… wala hatukutiliwa mkazo.”

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema juu yake katika “Majmuu´-ul-Fataawaa”:

“Makusudio yake inaweza kuwa kwamba makatazo hayakutiliwa mkazo, jambo ambalo halipingani na uharamu. Inawezekana vilevile yeye alidhani kuwa sio makatazo ya uharamu. Hoja iko katika maneno ya Mtume Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na si katika dhana ya mwengine.”[1]

[1] (24/355).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 67-69
  • Imechapishwa: 06/11/2019