Swali 33: Ni yepi maoni yako kuhusu kitabu “Qutbiyyah”? Unapendekeza kisomwe? Je, vitabu vya Ruduud ni katika mfumo wa Salaf (Rahimahumu Allaah)?

Jibu: Kuwaraddi wahalifu ni Sunnah ya Salaf. Salaf walikuwa wakiwaraddi wanaoenda kinyume. Vitabu vyao vipo. Imaam Ahmad aliwaraddi mazanadiki na wazushi. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah aliwaraddi wanafalsafa na watu wa mantiki, Suufiyyah na waabudia makaburi. Ibn-ul-Qayyim na maimamu wengine wengi waliwaraddi wanaoenda kinyume kwa ajili ya kuwabainishia watu haki ili ummah usipotee na ukawafuata wenye kukosea na wahalifu. Inahusiana na kuutakia ummah yaliyo mema.

Kuhusu kitabu “Qutbiyyah” na vyenginevyo, ni lazima kukubali haki iliyomo ndani. Ni kwa nini mtu asiraddiwe ikiwa mwenye kuraddi ananukuu vitabu vyake au kanda zake na anataja anwani ya vitabu, ukurasa na mjeledi? Malengo yao ni kuutakia ummah kheri na sio kuwatia watu upungufu. Wanachotaka ni kuwanasihi watu na kuwabainishia haki. Tatizo liko wapi muda wa kuwa kitabu “Qutbiyyah” au vyenginevyo havikuwazulia watu uwongo na badala yake vimenukuu maneno yao kama yalivyo kwa kutaja mjeledi, kurasa na hata msitari bila ya kutosheka na maana ya maandiko au mukhtaswari wa maneno ya yule aliyeenda kinyume?

Ni ghushi kwa ummah kuwaficha watu, kuwapaka watu mchanga wa machoni na kuwakimbiza vijana na watu kutokamana na vitabu hivi na kuwaambia kuwa vina sumu na makosa. Haijuzu kufanya hivo. Ni lazima kubainisha. Ni lazima kuamrisha mema na kukataza maovu. Pamoja na kuwa vitabu vya Ruduud vilikutwa tangu hapo kale hakuna yeyote aliyevikosoa na himdi zote njema ni za Allaah. Ni wajibu kubainisha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 90-91
  • Imechapishwa: 31/05/2023
  • mkusanyaji: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy