33. Ni sawa kusoma mazuri yaliyomo kwenye vitabu na mikanda ya wazushi?


Swali 33: Baadhi ya watu wanasema kuwa ni lazima kwako kuchukua kheri sawa iwe ni kutoka kwenye kitabu au mkanda na uache kosa liliyomo. Je, maneno haya ni sahihi na lini tunatakiwa kuanza kupima kati ya mazuri na mabaya? Je, msingi huu ni wa kimakosa? Tunaomba utuwekee wazi kwa kile unachoona kuwa ni munasibu.

Jibu: Kuhusiana na sentesi ya kwanza ni jambo lisilokuwa na shaka yoyote kwamba kheri inatakiwa kukimbiliwa. Lakini ukiwekewa sumu ndani ya asali unaweza kula na kunywa asali hii kwa madai kwamba kuna mazuri pamoja na kuwa ndani yake mna sumu? Jibu ni hapana kwa kuwa asali hii imechanganywa na kitu cha kukuangamiza.

Ambaye anatakiwa kufanya hivi ni yule ambaye anatambua kheri na awe vilevile anajua shari iliyomo ili ajitenge nayo. Katika hali hiyo hakuna neno. Kadhalika anaweza kuitenga mikanda hii kwa ajili ya kuikosoa na mfano wa hayo. Ama kusema kuwa atachukua ile kheri iliyomo, ilihali hajui na si muweza wa kupambanua baina ya kheri na shari, bila ya shaka ameenda kuiangamiza nafsi yake.

Kuhusiana na sentesi ya pili ya swalah ya kwamba ni lini inatakiwa kutendea kazi msingi wa kupima baina ya mazuri na mabaya, jibu ni kwamba kupima baina ya mazuri na mabaya sio jambo lililowekwa katika Shari´ah wakati wa kukosoa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuhusu Mu´aawiyah hana pesa kabisa na Abu Jahm ni mwenye kuwapiga wanawake.”

Amesema vilevile:

“Ibn Jamiyl hakuchukiwa isipokuwa alikuwa ni fakiri, basi Allaah akamtajirisha.”[1]

Hakutaja mazuri yao.

Kwa hivyo kujengea juu ya haya hakupimwi baina ya mazuri na mabaya. Uhakika wa mambo ni jambo lililozusliwa na watu wa Bid´ah.

[1] al-Bukhaariy (8585).