Ndugu wapendwa! Shari´ah ni hekima kutoka kwa Allaah na ni rehema ambayo Allaah amewarehemu waja Wake. Kwa sababu ni Shari´ah iliyojengeka juu ya wepesi na rehema inayotokana na usanifu na hekima. Allaah amemuwajibisha kila mmoja katika wale ambao ´ibaadah ni yenye kuwawajibikia kwa vile inavyonasibiana na hali yao ili kila mmoja aweze kutekeleza kile kinachomlazimu hali ya kukunjuka kifua chake na nafsi yenye kutulizana. Sambamba na hilo akiwa ni nwenye kumridhia Mola Wake, Uislamu kuwa dini yake na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Mtume Wake. Kwa hiyo waumini mshukuruni Allaah juu ya dini hii ilionyooka na juu ya yale aliyokuneemesheni kukuongozeni pale ambapo watu wengi wamepotea nayo. Mwombeni Allaah akuthibitisheni juu yake mpaka wakati wa kufa kwenu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 46
  • Imechapishwa: 25/04/2020