33. Dalili ya kwamba waumini watamuona Allaah kwa macho yao

33- Muhammad bin ´Aliy bin Muhammad as-Sunniy ametuhadithia: Muhammad bin Ibraahiym bin Naafiy´ ametuhadithia kwa kutusomea: Muusaa bin Haaruun ametuhadithia: Khalaf bin Hishaam ametuhadithia: Abuu Shihaab al-Hannaat ametuhadithia, kutoka kwa Ismaa´iyl bin Abiy Khaalid, kutoka kwa Qays bin Abiy Haazim, kutoka kwa Jariyr (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesema:

“Wakati mmoja tulikuwa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) safarini akautazama mwezi na kusema: “Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kwa macho kama mnavyouona mwezi mwandamo – hamtosongamana katika kumuona huko. Iwapo mtaweza kuswali kabla ya jua kuchomoza na kabla ya jua kuzama basi fanyeni hivo.” Kisha akasoma:

وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ

“Sabihi kwa himdi za Mola wako kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama.” (50:39)

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 72
  • Imechapishwa: 08/02/2017