33. Dalili juu ya kucheka kwa Allaah

32- ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Abdil-´Aziyz ametuhadithia: Hudbah bin Khaalid Abu Khaalid al-Qaysiy ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa Ya´laa bin ´Atwaa’, kutoka kwa Wakiy´ bin Hudus, kutoka kwa Abu Raziyn aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wetu (´Azza wa Jall) anacheka juu ya kukata tamaa kwa waja Wake pamoja na kuwa mageuzo Yake yalikuwa karibu.” Nikasema: “Mola (´Azza wa Jall) anacheka?” Akasema: “Ndio.” Ndipo nikasema: “Basi Mola ambaye anacheka kamwe hatotunyima kheri.”[1]

[1] at-Twayaalisiy (1092), Ahmad (4/11), Ibn Maajah (181), Ibn Abiy ´Aaswim (554), at-Twabaraaniy (19/207), al-Aajurriy, uk. 279, na ad-Daaraqutwniy (30). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Silsilat-ul-Ahaadîth as-Swahiyhah” (6/2/732-733).

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 72-73
  • Imechapishwa: 02/03/2018